Strängnäs inaanzisha tena ushirikiano na kijiji cha Wamasai Emboreet nchini Tanzania

Manispaa ya Strängnäs nchini Uswidi kwa muda mrefu imekuwa ikishiriki katika ushirikiano wa manispaa juu ya maudhui ya ushawishi wa vijana na washirika mbalimbali nchini Tanzania. Manispaa sasa inaanzisha upya ushirikiano na kijiji cha Maasai Embooret, asante ICLD kwa ruzuku.

Katika wilaya ya Simanjiro kaskazini mwa Tanzania, kuna kijiji cha Wamasai cha Emboreet, kijiji ambacho manispaa ya Strängnäs ilikuwa na ushirikiano wa manispaa kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2016. Wakati huo, baraza la wanafunzi lilianzishwa katika shule ya msingi ya kijiji hicho, ambalo linafanya kazi vizuri hadi leo. Maboresho kadhaa yamefanywa shuleni tangu kuanzishwa kwa baraza la wanafunzi wakati huo, mfano kusimikwa kwa umeme wa jua, na mambo mengine pia. Karibu na kijiji cha Simanjiro kuna shule ya sekondari, ambayo wanafunzi wameunda klabu ya  hali ya hewa  ambayo hufanyika wakati wa saa za shule. Katika kijiji hicho, pia kuna kikundi imara cha  wanawake wanaofanya kazi kwa ajili ya jamii endelevu. 

Kupitia ushirikiano wetu ulioanzishwa upya, sasa tunataka kufanya kazi ili kuimarisha dhamira ya wanawake na, kwa kushirikiana na mawazo ya wanafunzi, kuleta uboreshaji wa mazingira katika kijiji, anasema Helena Edvinsson ambaye ni kamishna wa haki za watoto katika manispaa ya Strängnäs na meneja wa mradi wa ushirikiano na Emboreet.

Strängnäs inaona fursa kwa manispaa yake yenyewe, kwa msaada wa ushirikiano, kuandaa mahali pa kukutana katikati mwa mji ambapo manispaa inaweza kutumia ujuzi kutoka kwa ushirikiano kati ya kikundi cha wanawake na wanafunzi wa shule hizo mbili, ili kupata mahali pa mikutano ya manispaa ambayo inapatikana kwa wote.

“Hivi sasa, tunaendelea na mchakato wa kuainisha changamoto za kidemokrasia ambazo ushirikiano wetu wa pamoja utafanyia kazi. Inaegemea katika uendelevu wa kijamii ulioboreshwa pamoja na hitaji la kukuza maeneo ya mikutano,” anasema Helena Edvinsson.

Majibu ya moja kwa moja katika kijiji cha Wamasai

Helena pia anazungumzia mafunzo waliyopata kutokana na ushirikiano wao wa awali na kijiji cha Wamasai ambao bado unawasaidia hadi leo. Miongoni mwa mambo mengine, jinsi mikutano yao kati ya watoto na watoa maamuzi imekuwa rahisi, wazi na yenye ufanisi zaidi.

Strängnäs kwa miaka kadhaa wamefanya kongamano la watoto na vijana, ambapo wanasiasa walifanya vikao vya asubuhi ili kuwapa watoto majibu ya maswali yao kuhusu mada mbalimbali. Lilikuwa tukio zuri, lakini maswali mengi bado yasingejibiwa mwisho wa siku. Jibu linaweza kuwa “Nitawasilisha swali” kutoka kwa wanasiasa waliopokea maswali ambayo hayakuhusu eneo lao la kuwajibika. Kwa upande mwingine – katika kijiji cha Wamasai – kijiji kizima kilikusanyika kujibu maswali ya watoto. Hakuna “aliyewasilisha swali” kwa sababu wanasiasa wote waliowajibika walikuwepo. Watoto walipokea jibu mara moja! Kwa uzoefu toshelevu zaidi, manispaa ya Strängnäs ilibadilisha muundo na kumaliza kongamano la watoto na vijana. Badala yake, mikutano ya mada inafanyika leo ambapo wale wote wanaohusika wanahudhuria. Watoto hupata jibu mara moja!

ICLD inawatakia wote mafanikio mema na inatarajia mafanikio juu ya safari yao ya demokrasia!

Translated by ICLD intern Oliver Kadushi.